Biblia inasema nini juu ya udhibiti wa idadi ya watu?

Swali Biblia inasema nini juu ya udhibiti wa idadi ya watu? Jibu Biblia haisemi chochote kuhusu udhibiti wa idadi ya watu. Badala yake, wanadamu wanaambiwa “Zaeni, mkaongezeke” (Mwanzo 1:22, 28). Zaburi 127: 3-5 inatuambia kwamba watoto ni urithi kutoka kwa Bwana na kwamba uzao wa tumbo ni zawadi kutoka kwake. Wakati wa maandishi haya, kuna…

Swali

Biblia inasema nini juu ya udhibiti wa idadi ya watu?

Jibu

Biblia haisemi chochote kuhusu udhibiti wa idadi ya watu. Badala yake, wanadamu wanaambiwa “Zaeni, mkaongezeke” (Mwanzo 1:22, 28). Zaburi 127: 3-5 inatuambia kwamba watoto ni urithi kutoka kwa Bwana na kwamba uzao wa tumbo ni zawadi kutoka kwake.

Wakati wa maandishi haya, kuna watu takriban bilioni 7.1,000,000 duniani. Kuna mita za mraba trilioni 7.5 za ardhi katika jimbo laTexas, huko Marekani, pekee. Hii ina maana kwamba, kwa kinadharia, kila mtu duniani anaweza kutoshea katika jimbo la Texas, na kila mtu atakuwa mita mraba 1,056 ya nafasi ya kuishi- 4,224 kwa familia ya watu wanne! Tunaweza kusema kuwa tatizo siyo idadi ya watu lakini ni ukosefu wa rasilimali (chakula, maji, nk) na uwezo wa kugawa rasilimali hiyo.

Ikiwa watu wote duniani wanaweza kutoshea huko Texas, kuna nafasi nyingi ingebaki ikiwa watu watatawanyika katika majimbo yote ya Marekani. Hii itawawezesha nafasi kubwa ya kuishi pamoja na upatikanaji wa maji, ardhi ya kilimo, barabara na miundombinu nyingine.

Bila shaka, kuna maeneo huko Marekani ambayo binadamu hawezi kuishi. Hata hivyo, kuna maeneo mengi ulimwenguni pote yenye ardhi bora ya kilimo na maji safi ya kunywa. Kwa kweli, idadi ya watu haiitaji “kudhibitiwa.”

Wale wanaotetea udhibiti wa idadi ya watu kwa kawaida hutumia njia ovu, kama vile utoaji mimba, kufisha bila maumivu, na utasa wa kulazimisha. Mipango kama vile kulazimisha kuavya mimba moja kwa moja inapingana na mafundisho ya Biblia kwamba maisha ya mwanadamu ni takatifu. Wahamasishaji wa udhibiti wa idadi ya watu huzingatia sera ambazo zinasisitiza kwamba tatizo ni wanadamu wengi, ilhali tatizo halisi limepuuzwa.

Tatizo si ukubwa wa idadi ya watu wala uhaba wa rasilimali. Tatizo ni dhambi. Watu wenye ubinafsi, wenye dhambi, na wenye tamaa za mamlaka wametumia vibaya viumbe vya Mungu. Mungu alitaka binadamu awe na mamlaka juu ya viumbe vingine (Mwanzo 1:26). Wanadamu wangepaswa kuwa wasimamizi wa dunia, na 1 Wakorintho 4: 2 inaongezea kwamba ” Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu .” Kwa kusikitisha, serikali zenye ufisadi, badala ya kuwa waaminifu na rasilimali za nchi, mara nyingi huwa dudnuliza chakula, kupoteza rasilimali, na kuiba pesa badala ya kushugulikia wananchi. Makampuni makubwa, pia, wanajitahidi kudhibiti zaidi na zaidi ya ugavi wa chakula na wanaonekana kuwa tayari kutoa michuano ya faida kuliko kufaidi jamii.

Jibu la kibiblia kwa “idadi kubwa zaidi” sio kuwahitaji watu wachache. Ni kuwaheshimu watu na kushugulikia mahitaji yao (tazama Marko 12:31). Tamaa ya mamlaka, na upumbavu husababisha matumizi mabaya ya rasilimali, na kwa hivyo mamilioni ya watu wanateseka.

[English]



[Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili]

Biblia inasema nini juu ya udhibiti wa idadi ya watu?

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.