Biblia inasema nini kuhusu woga?

Swali Biblia inasema nini kuhusu woga? Jibu Biblia inafunza wazi wazi kwamba Wakristo hawapaswi kuwa na woga. Katika Wafilipi 4: 6, tunaamuriwa, “Msijisumbue kwa neno lo lote bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru haja zenu na zijulikane na Mungu” Katika andiko hili, tunajifunza kwamba lazima tulete mahitaji yetu yote na…

Swali

Biblia inasema nini kuhusu woga?

Jibu

Biblia inafunza wazi wazi kwamba Wakristo hawapaswi kuwa na woga. Katika Wafilipi 4: 6, tunaamuriwa, “Msijisumbue kwa neno lo lote bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru haja zenu na zijulikane na Mungu” Katika andiko hili, tunajifunza kwamba lazima tulete mahitaji yetu yote na wasiwasi kwa Mungu katika maombi badala ya kujisumbua kwayo. Yesu anatutia moyo ili kuepuka hofu juu ya mahitaji yetu ya kimwili kama vile nguo na chakula. Yesu anatuhakikishia kwamba Baba yetu wa mbinguni Atahudumia mahitaji yetu yote (Mathayo 6: 25-34). Kwa hiyo, hatuna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu kitu chochote.

Tangu hofu haipaswi kuwa sehemu ya maisha ya muumini, jinsi gani mtu anaishinda wasiwasi? Katika 1 Petro 5: 7 tunaelezwa “Huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maan yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu” Mungu hataki tubeba kote mzigo wa matatizo na mizigo. Katika mstari huu, Mungu anatueleza tumpe woga wetu wote na wasiwasi. Kwa nini Mungu Anataka kutubebea matatizo yetu? Biblia inasema ni kwa sababu Yeye anatujali. Mungu ni wasiwasi kuhusu kila kitu kinachotokea kwetu. Hakuna wasiwasi ni kubwa mno au ndogo mno kwa ajili ya tahadhari yake. Wakati sisi kumpa Mungu matatizo yetu, ameahidi kutupa amani ipitayo akili zote (Wafilipi 4: 7).

Bila shaka, kwa wale ambao hawamjui Mwokozi, woga na wasiwasi utakuwa ni sehemu ya maisha. Lakini kwa wale ambao wametoa maisha yao kwake, Yesu aliahidi, “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha katika nafsini mwenu. Kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi” (Mathayo 11: 28-30).

[English]



[Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili]

Biblia inasema nini kuhusu woga?

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.