Je! Dhambi ya Adamu na Hawa ilikuwa kweli juu ya kula kipande cha tunda iliyokatazwa?

Swali Je! Dhambi ya Adamu na Hawa ilikuwa kweli juu ya kula kipande cha tunda iliyokatazwa? Jibu Maneno “Tunda lililokatazwa”linahusu hadithi ya Adamu na Hawa katika bustani ya Edeni. Walikatazwa na Mungu kula tunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya (Mwanzo 2: 9, 3: 2). Biblia haisemi chochote kuhusu aina gani ya tunda…

Swali

Je! Dhambi ya Adamu na Hawa ilikuwa kweli juu ya kula kipande cha tunda iliyokatazwa?

Jibu

Maneno “Tunda lililokatazwa”linahusu hadithi ya Adamu na Hawa katika bustani ya Edeni. Walikatazwa na Mungu kula tunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya (Mwanzo 2: 9, 3: 2). Biblia haisemi chochote kuhusu aina gani ya tunda . kitamaduni tunda hilo linatambulika kama tufaha, lakini haiwezekani kujua kwa uhakika lilikua ni aina gani ya tunda. Kutoka kwenye maandishi ya Mwanzo, inaashiria kuwa ni mti halisi wenye matunda halisi.

Kipengele muhimu katika kifungu hicho sio tunda lenyewe, bali ni marufuku dhidi ya kulila. Mungu aliwakataza Adamu na Hawa kitu kimoja tu katika maagizo Yake. Ikiwa kulikuwa na mali fulani ya kiroho ndani ya matunda, hio haina uhusioano wowote. Dhambi ilikuwa katika kutotii amri ya Mungu. Kwa kula tunda (kitendo cha kutotii), Adamu na Hawa walipata ujuzi wa kibinafsi juu ya uovu. Walikuwa tayari wanajua mema, lakini sasa walikuwa na uzoefu tofauti wa uovu wa kutotii na hatia na aibu ambayo ilikuja nayo. Uongo wa Shetani ni kwamba kujua mema na mabaya kungewafanya kuwa miungu (Mwanzo 3: 5). Kwa kweli, walikuwa tayari wameumbwa kwa mfano wa Mungu na walikuwa na baraka ya furaha yake nzuri.

Somo kwetu sisi leo ni kwamba wakati Mungu anazuia kitu fulani, ni kwa manufaa yetu wenyewe. Kutomtii, kwenda kwa njia yetu wenyewe, au kujiamulia wenyewe kilicho na kisicho na manufaa kwetu daima husababisha janga. Baba yetu wa mbinguni ambaye alituumba sisi anajua kilicho chema kwetu sisis na wakati anakataza kitu fulani, tunapaswa kumsikiliza. Tunapochagua kutii mapenzi yetu wenyewe badala ya mapenzi yake kamili na matakatifu, mambo hayatendei vizuri. Adamu na Hawa walifanya ugunduzi huo wa kusikitisha baada ya kula tunda lililokatazwa, na wanadamu wamepata kuteseka juu ya matokeo ya uamuzi wao tangu wakati huo (Warumi 5:12).

[English]



[Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili]

Je! Dhambi ya Adamu na Hawa ilikuwa kweli juu ya kula kipande cha tunda iliyokatazwa?

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *