Je, hoja ya Ontolojia ya kuwepo kwa Mungu ina maana gani?

Swali Je, hoja ya Ontolojia ya kuwepo kwa Mungu ina maana gani? Jibu hoja ya ontolojia ni hoja isiyozinduliwa kwa uchunguzi wa dunia (kama hoja za kiroholojia na za kiteolojia) lakini imesababishwa fa fikra pekee. Hasa, hoja ya ontolojia yatokana na utafiti wa ontoloji (ontology). Fomu ya kwanza na maarufu zaidi ya hoja hii yatoka…

Swali

Je, hoja ya Ontolojia ya kuwepo kwa Mungu ina maana gani?

Jibu

hoja ya ontolojia ni hoja isiyozinduliwa kwa uchunguzi wa dunia (kama hoja za kiroholojia na za kiteolojia) lakini imesababishwa fa fikra pekee. Hasa, hoja ya ontolojia yatokana na utafiti wa ontoloji (ontology). Fomu ya kwanza na maarufu zaidi ya hoja hii yatoka kwa St. Anselm katika karne ya 11 A.D. Anaanza kwa kusema kuwa dhana ya Mungu ni kwamba ‘ hakuna kingine kitakachozinduliwa kizidi ukuu wa Mungu.” Kwa kuwa kuwepo kunawezekana, na kuwepo ni ukuu zaidi kuliko kutowepo, basi Mungu lazima awepo (kama Mungu hakuwapo, basi mtu mkubwa anaweza kuzaliwa, lakini hiyo ni kujiadaa mwenyewe kwa sababu huwezi kuwa na kitu kikubwa zaidi kuliko kile hakuna mkuu anayeweza kuzaliwa au kugunduliwa!). Kwa hivyo, Mungu lazima awepo. Descartes alielezea jambo sawa na hili ila tu, alianza na wazo la Mtu ambaye hana kosa lolote.

Bertrand Russell ambaye, hamwamini Mungu alisema kuwa ni rahisi sana kusema kuwa hoja ya ontolojia si nzuri kuliko kueleza hitilafu yake ni nini haswa! Hata hivyo, hoja za ontolojia hazijulikani sana katika miduara ya Kikristo nyingi siku hizi. Kwanza, wanaonekana kuwaza kuhusu asili ya Mungu au vile Mungu anavyofanana. Pili, rufaa ya kujitegemea ni ya chini kwa wasiokuwa waumini, kwa kuwa hoja hizi huwa zinakosa lengo halisi. Tatu, ni vigumu tu kusema kwamba kitu lazima kiwepo kwa ufafanuzi. Bila kuungwa mkono na filosofi nzuri katika kuelezea ni kwa nini kitu kinapaswa kuwepo, kufafanua tu uwepo wa kitu fulani sio falsafa nzuri . Ingawa kuna Matatizo mengi, wanafilosofia kadhaa maarufu leo wanaendelea kuifanyia kazi hoja hiii ya kitheolojia isiyo ya kawada.

[English]


[Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili]

Je, hoja ya Ontolojia ya kuwepo kwa Mungu ina maana gani?

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.