Je, ninawezaje kujua ikiwa ninamsikia Mungu, namsikia Shetani, au ninasikia mawazo yangu?

Swali Je, ninawezaje kujua ikiwa ninamsikia Mungu, namsikia Shetani, au ninasikia mawazo yangu? Jibu Maisha yamejaa maamuzi ambayo hayana maelekezo kamili, hususani kwa jina, jinsi ya kupata katika Biblia. Je! kwa siku watoto wangu wanafaa kutumia muda mgani katika runinga? Je, ni bora kucheza michezo fulani ya kanda? Je, ninaruhusiwa kuchumbiana na mfanyakazi mwenzangu? Je,…

Swali

Je, ninawezaje kujua ikiwa ninamsikia Mungu, namsikia Shetani, au ninasikia mawazo yangu?

Jibu

Maisha yamejaa maamuzi ambayo hayana maelekezo kamili, hususani kwa jina, jinsi ya kupata katika Biblia. Je! kwa siku watoto wangu wanafaa kutumia muda mgani katika runinga? Je, ni bora kucheza michezo fulani ya kanda? Je, ninaruhusiwa kuchumbiana na mfanyakazi mwenzangu? Je, ni sawa kukosa kwenda kazini kwa sababu nilikesha usiku wa kuamkia? Sisi wote tuna mawazo kuhusu ukweli, lakini tunajuaje kwa uhakika kwamba mawazo haya yanatoka kwa Mungu? Je, ninasikia Mungu? Au labda najisikiza mimi mwenyewe? Baya zaidi, nasikiza majaribu ya Shetani kana kwamba ni uongozi wa Roho Mtakatifu? Wakati mwingine kutofautisha mawazo yetu wenyewe kutoka kwa uongozi wa Mungu ni vigumu. Na itakuwaje ikiwa misukumo yetu inatoka kwa adui na nafsi zetu na sio kwa Mungu? Je, tunawezaje, “tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo” (2 Wakorintho 10:5) wakati hatuna uhakika ni mahali gani mawazo yanatoka?

Mara nyingi kwa kawaida, Mungu huwasiliana kupitia Biblia, Neno Lake lilioongozwa na roho, limehifadhiwa kwa karne nyingi kwa ajili yetu hii leo. Ni kupitia Neno tunatakaswa (Yohana 17:17), na Neno ndilo nuru ya njia yetu (Zaburi 119:105). mungu pia anaweza kutuongoza kupitia hali (2 Wakorintho 2:12), maongozi ya Roho (Wagalatia 5:16) na washauri wa kimungu wakitoa ushauri wa hekima (Mithali 12:15). Ikiwa Mungu anataka kuzungumza nasi, hakuna kinachoweza kumzuia. Hapa kunazo baadhi ya njia unaweza kubambanua chanzo cha mawazo yetu:

Maombi

Ikiwa tunachanganyikiwa kuhusu kama tunamsikia Mungu au la, ni vyema kuomba kwa ajili ya hekima (Yakobo 1:5). (Ni vyema kuomba hekima hata wakati hatufikirii kuwa tumechanganyikiwa!) Tunapaswa kumuuliza Mungu afanye mapenzi yake kwa wazi yajulikane kwetu. Wakati tunaomba “lazima aamini wala asiwe na shaka, kwa sababu mtu aliye na shaka ni kama wimbi la bahari, lililochukuliwa na upepo na kutupwa huku na huku” (Yakobo 1:6). Ikiwa hatuna imani, “Mtu kama huyo asidhani ya kuwa atapata kitu chochote kutoka kwa Bwana” (Yakobo 1:7).

Zungumza na Mungu kwa maombi na ungojee jibu lake kwa hamu. Walakini, kumbuka kwamba Mungu hatupi kila kitu tunachotamani, na wakati mwingine jibu Lake ni “Hapana.” Anajua kile tunachohitaji wakati wowote, na atatuonyesha kilicho bora zaidi. Ikiwa Mungu atasema, “La,” basi tunaweza kumshukuru kwa uwazi wa mwelekezo Wake na kuendelea kutoka hapo.

Soma Neno

Biblia inaitwa “Neno la Mungu” kwa sababu fulani-ndio njia ya msingi Mungu huzungumza nasi. Pia ni njia ambayo tunajifunza tabia ya Mungu na kazi Yake kwa watu katika historia. Kila Andiko ni “pumzi ya Mungu” na ni mwongozo wa maisha ya haki (2 Timotheo 3:16-17). Tunazungumza na Mungu kwa maombi, Yeye huzungumza nasi kupitia Neno Lake. Tunaposoma, ni lazima tuchukulie maneno ya Biblia kuwa maneno ya Mungu mwenyewe.

Wazo lolote, tamaa, pendeleo au msukumo wowote tunaweza kuwa nao lazima ulinganishwe na Neno la Mungu na ukubaliwe. Wacha Biblia iwe mwamuzi wa kila wazo. “Kwa maana Neno la Mungu li hai tena lina nguvu. Lina makali kuliko upanga wowote wenye makali kuwili, hivyo linachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, viungo na mafuta yaliyo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo” (Waebrania 4:12). Haijalishi uharaka wa msukumu, lakini kama unaenda kinyume na vile Maandiko yasemavyo, basi msukumu huo sio wa Mungu na lazima ukataliwe.

Fuata uongozi wa Roho Mtakatifu

Roho Mtakatifu ni Mungu-kiumbe cha kimungu chenye akili, hisia, na mapenzi. Yeye daima yuko nasi (Zaburi 139:7-8). Majukumu yake ni pamoja na kutuombea (Warumi 8:26-27) na kupeana karama za kulinufaisha kanisa (1 Wakorintho 12:7-11).

Roho Mtakatifu anataka kutujaza (Waefeso 5:18) na kukuza matunda ndani yetu (Wagalatia 5:22-25). Haijalishi ni maamuzi gani tunayofanya siku baada ya siku, hatuwezi kukosea tunapoonyesha upendo, furaha, amani, n.k., kwa utukufu wa Mungu. Tunapokuwa na wazo la nasibu kichwani mwetu, lazima tujifunze “kuzijaribu roho” (1 Yohana 4:1). Je! kufuata mwelekeo huo kutatufanya tufanane na Kristo? Je! kudumu katika wazo hili kutazalisha zaidi tunda la Roho ndani yangu? Roho Mtakatifu hawezi kutuongoza kamwe kutimiza tamaa za dhambi za kimwili (Wagalatia 5:16); kila mara atatuongoza kwa utakaso (1 Petro 1:2). Maisha katika dunia ni vita vya kiroho. Adui ako na hamu ya kutupa vipotovu ili kutukengeusha kutoka kwa mapenzi ya Mungu (1 Petro 5:8). Ni lazima tuwe macho ili kuhakikisha kwamba kile tunachotii ni zaidi ya hisia na kwa kweli kinatoka kwa Mungu mwenyewe.

Kumbuka, Mungu anataka kutuonyesha njia sahihi ya kufuata. Mungu hafichi mapenzi yake kutoka kwa wale wanaomtafuta.

Hapa kuna baadhi ya maswali mazuri ya kuuliza tunapochunguza kama tunamsikia Mungu au la: Je, misukumo hiyo inachanganya au ina utata? Mungu si mwanzilishi wa machafuko; Yeye ndiye mleta amani (1 Wakorintho 14:33). Je mawazo yanapingana na Neno la Mungu? Mungu hajichanganyi Mwenyewe. Je, kufuata maongozi haya kutasababisha dhambi? Wale ambao “wanaenenda kwa Roho” “wameusulubisha mwili na shauku zake pamoja na tamaa zake” (Wagalatia 5:24-25).

Fauka ya hayo, ni vyema kutafuta ushauri kutoka kwa rafiki Mkristo, mwanafamilia, au mchungaji (Mithali 15:22). Wachungaji wetu wapo ili kusaidia kutuchunga: “Watiini viongozi wenu na kujinyenyekeza chini ya mamlaka yao. Kwa maana wao wanakesha kwa ajili yenu kama watu watakaopaswa kutoa hesabu” (Waebrania 13:17).

Mungu hataki tuanguke. Kadri tunavyomsikiliza Mungu, ndivyo tutakavyokuwa bora zaidi katika kutofautisha sauti yake na kelele zingine katika vichwa vyetu. Yesu Mchungaji Mwema, anatoa ahadi yake: “Akiisha kuwatoa wote nje, hutangulia mbele yao na kondoo humfuata kwa kuwa wanaijua sauti yake” (Yohana 10:4). Wengine wanaweza kuzungumza, “lakini kondoo hawakuwasikia” (aya ya 8). Kidri tunavyomjua Mchungaji wetu, ndipo tutaacha kuwa na wasiwasi kuhusu kusikiza sauti isiyofaa.

[English]



[Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili]

Je, ninawezaje kujua ikiwa ninamsikia Mungu, namsikia Shetani, au ninasikia mawazo yangu?

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.