Je, tunapaswa kutoa zaka kutoka kwa jumla ya mapato yetu au mapato baada faida?

Swali Je, tunapaswa kutoa zaka kutoka kwa jumla ya mapato yetu au mapato baada faida? Jibu Zaka ni dhana ya Agano la Kale. Zaka ilikuwa hitaji la sheria ambapo Waisraeli wote walipaswa kutoa asili mia kumi (10%) ya kila kitu walichomiliki-au mazao waliokuza na mifugo waliofuga-kwenye Hema la Kukutania/Hekalu (Walawi 27:30; Hesabu 18:26; Kumbukumbu 14:24;…

Swali

Je, tunapaswa kutoa zaka kutoka kwa jumla ya mapato yetu au mapato baada faida?

Jibu

Zaka ni dhana ya Agano la Kale. Zaka ilikuwa hitaji la sheria ambapo Waisraeli wote walipaswa kutoa asili mia kumi (10%) ya kila kitu walichomiliki-au mazao waliokuza na mifugo waliofuga-kwenye Hema la Kukutania/Hekalu (Walawi 27:30; Hesabu 18:26; Kumbukumbu 14:24; 2 Mambo ya Nyakati 31:5). Waumini katika Kristo hawajaamrishwa kutoa 10% ya mapato yao. Kila Mkristo anapaswa kuomba kwa hekima, na kutafuta hekima ya Mungu ya ni kiasi kigani anaweza kutoa (Yakobo 1:5). Watu wengi wanaamini kwambazaka ya Agano la Kale ni kanuni nzuri kwa waumini kufuata. Kutoa 10% ya mapato yako kwa Mungu kunaonyesha shukrani yako kwake kwa kila alichokupa nakukusaidia kukumbuka kumtegemea Mungu badala ya utajiri.

Biblia haisemi haswa ikiwa tunapaswa kutoa 10% ya mapato yetu yote au mapato baada ya kutozwa ushuru. Agano la Kale linafunza kanuni ya malimbuko (Kutoka 23:16; 34:22; Walawi 2:12-14; 2 Mambo ya Nyakati 31:5). Waumini wa Agano la Kale walitoa mazao bora zaidi kutoka kwa mimea yao, na sio mabakishishi. Kanuni yiyo hiyo inapaswa kutumika katika matoleo yetu hii leo. Tena, muumini anapaswa kutoa kile anachoamini kwamba Mungu anamtaka atoe. Katika yote, nia ya moyo ndio hujalisha. Je, tunatoa kwa kumcha Mungu au kwa ubinafsi kwa ajili ya mali zetu wenyewe? ”Kila mtu atoe kama anavyokusudia moyoni mwake, si kwa uchoyo au kwa kulazimishwa, kwa maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu” (2 Wakorintho 9:7).

[English]



[Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili]

Je, tunapaswa kutoa zaka kutoka kwa jumla ya mapato yetu au mapato baada faida?

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.