Kitabu cha 2 Wathesalonike

Kitabu cha 2 Wathesalonike Mwandishi: 2 Wathesalonike 1: 1 inaonyesha kuwa kitabu cha 2 Wathesalonike kiliandikwa na Mtume Paulo, pengine pamoja na Sila na Timotheo. Tarehe ya kuandikwa: kitabu cha 2 Wathesalonike huenda kiliandikwa katika 51-52 BK. Kusudi la Kuandika: kanisa la Thesalonike bado lilikuwa na baadhi ya uelewa visivyo kuhusu Siku ya Bwana. Waidhani…

Kitabu cha 2 Wathesalonike

Mwandishi: 2 Wathesalonike 1: 1 inaonyesha kuwa kitabu cha 2 Wathesalonike kiliandikwa na Mtume Paulo, pengine pamoja na Sila na Timotheo.

Tarehe ya kuandikwa: kitabu cha 2 Wathesalonike huenda kiliandikwa katika 51-52 BK.

Kusudi la Kuandika: kanisa la Thesalonike bado lilikuwa na baadhi ya uelewa visivyo kuhusu Siku ya Bwana. Waidhani ilikuwa imekuja tayari hivyo wakaacha kazi zao. Walikuwa wakiteswa vibaya. Paulo aliandika kutoa kutoelewa vibaya na kuwafariji.

Mistari muhimu: 2 Wathesalonike 1: 6-7, “Kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi; na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake.”

2 Wathesalonike 2:13, “Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli.”

2 Wathesalonike 3: 3, “Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu.”

2 Wathesalonike 3:10, “Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.”

Muhtasari kwa kifupi: Paulo anasalimia kanisa katika Thesalonike na kuwatia moyo na kuwahimiza. Anawapongeza kwa kile anasikia wanafanya katika Bwana, na anawaombea (2 Wathesalonike 1: 11-12). Katika sura ya 2, Paulo anaeleza nini kitatokea katika siku ya Bwana (2 Wathesalonike 2: 1-12). Paulo kisha anawahimiza kusimama imara na kuwaelekeza wajitenge na watu wavivu ambao hawaishi kwa injili (2 Wathesalonike 3: 6).

Mashirikisho: Paulo anarejelea vifungu kadhaa katika Agano la Kale katika mahubiri yake juu ya nyakati za mwisho, na hivyo kuthibitisha na kuwapatanisha manabii wa Agano la kale. Mengi ya mafundisho yake juu ya nyakati za mwisho katika barua hii yana misingi kwa nabii Danieli na maono yake. Katika 2 Wathesalonike 2: 3-9, anarejelea unabii wa Danieli kuhusu “mtu wa dhambi” (Danieli 7-8).

Vitendo Tekelezi: Kitabu cha 2 Wathesalonike kumejazwa na habari ambayo inaelezea nyakati za mwisho. Pia hutuhimiza tusiwe wavivu na kufanya kazi kwa kile tulicho nacho. Pia kuna maombi makuu katika 2 Wathesalonike ambayo yanaweza kuwa mfano kwetu juu ya jinsi ya kuomba kwa ajili ya waumini wengine siku hizi.

[English]



[Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili]

Kitabu cha 2 Wathesalonike

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.