Ni kitu gani kitaenda kutendeka kulingana na unabii wa nyakati za mwisho?

Swali Ni kitu gani kitaenda kutendeka kulingana na unabii wa nyakati za mwisho? Jibu Bibilia iko na mengi ya kusema kuhusu nyakati za mwisho. Karibu kila kitabu cha Bibilia kiko na unabii kuhusu nyakati za mwisho. Kusungumzia huu unabii na kuupanga waweza kuwa kazi ngumu. Ufuatao ni mukhutasari kuhusu ni nini Bibilia inasema kitatokea katika…

Swali

Ni kitu gani kitaenda kutendeka kulingana na unabii wa nyakati za mwisho?

Jibu

Bibilia iko na mengi ya kusema kuhusu nyakati za mwisho. Karibu kila kitabu cha Bibilia kiko na unabii kuhusu nyakati za mwisho. Kusungumzia huu unabii na kuupanga waweza kuwa kazi ngumu. Ufuatao ni mukhutasari kuhusu ni nini Bibilia inasema kitatokea katika nyakati za mwisho.

Kristo atawatoa wote ambao wameokoka kutoka ulimwengu kwa tukio lijulikanalo kama unyakuzi (1 Wathesalonike 4:13-18; 1 Wakorintho 15:51-54). Katika kiti cha enzi cha Kristo, hawa wateule watapewa taji kwa kazi yao na uaminifu wa kazi yao wakati walikua ulimwenguni ama wataipoteza taji, bali si uzima wa milele, kwa kukosa huduma na unyenyekevu (1 Wakorintho 3:11-15; 2 Wakorintho 5:10).

Mpinga Kristo (joka) atakuja mamlakani na ataweka mkataba na Israeli kwa kipindi cha miaka saba (Danieli 9:27). Hiki kipindi cha miaka saba kinaitwa “matezo.” Wakati wa matezo kutakua na vita vya kuogofya, njaa, mapigo, na majanga. Mungu ataimwaga ghadhabu yake kwa dhambi, maovu na hali yoyote ya kuasi. Matezo yatajumlisha kuoneka kwa farasi wane wa kimafumbo, na mihuri saba, tarumbeta saba na ghala la hukumu.

Kwa muda nusu wa kipindi cha miaka saba, mpinga Kristo atavunja agano la amani na Israeli na kufanya vita na Israeli. Mpinga Kristo atafanya “maovu yasiyo kubaliwa” na kuweka mfano wake uabudiwe katika hekalu la Yerusalemu (Danieli 9:27; 2 Wathesalonike 2:3-10), ambayo ilikua imekwisha jengwa. Kipindi kingine nusu cha matezo kinaitwa “matezo makuu” (Ufunuo Wa Yohana 7:14) na “wakati wa matezo ya Yakobo” (Yeremia 30:7).

Mwisho wa matezo ya miaka saba, yule mpinga Kristo ataunda kikosi cha kufamia Yerusalemu, vikianzisha vita vya Amagedo. Yesu Kristo atarudi, na amwangamize mpingamizi na jeshi lake na kuwatupa katika tanuru la moto (Ufunuo Wa Yohana 19:11-21). Kisha Kristo atamfunga Shetani kuzimu miaka 1000 atatawala dunia yake kwa hiki kipindi cha miaka elfu moja (Ufunuo Wa Yohana 20:1-6).

Mwisho wa miaka elfu moja, shetani atafunguliwa na kushindwa tena na kutupwa katika tanuru la moto (Ufunuo Wa Yohana 20:7-10) milele yote. Kristo kisha atawahukumu wote walioasi (Ufunuo Wa Yohana 20:10-15) kitika kiti kieupe cha hukumu, akiwatupa wote katika tanuru la moto. Kristo kisha ataikaribisha mbingu mpya, nchi mpya na Yerusalemu mpya-mahali pa milele pa wateule wataishi. Hakutakuwa na dhambi tena, husuni wala kifo (Ufunuo Wa Yohana 21-22).

[English]



[Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili]

Ni kitu gani kitaenda kutendeka kulingana na unabii wa nyakati za mwisho?

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.