Ni nani aliyekuwa mtu mkongwe zaidi katika Biblia?

Swali Ni nani aliyekuwa mtu mkongwe zaidi katika Biblia? Jibu Mwanzo mlango wa 5 inaorodhesha wanaume tisa ambao walikuwa na maisha marefu. Jinsi na kwa nini waliishi maisha marefu kama hayo haijasemwa haswa. Adamu aliishi miaka 930 (Mwanzo 5:5). Sethi aliishi miaka 912(Mwazo 5:8). Enoshi aliishi miaka 905 (Mwanzo5:11). Kenani aliishi miaka 910 (Mwanzo 5:14)….

Swali

Ni nani aliyekuwa mtu mkongwe zaidi katika Biblia?

Jibu

Mwanzo mlango wa 5 inaorodhesha wanaume tisa ambao walikuwa na maisha marefu. Jinsi na kwa nini waliishi maisha marefu kama hayo haijasemwa haswa. Adamu aliishi miaka 930 (Mwanzo 5:5). Sethi aliishi miaka 912(Mwazo 5:8). Enoshi aliishi miaka 905 (Mwanzo5:11). Kenani aliishi miaka 910 (Mwanzo 5:14). Mahaleli aliishi miaka 895 (Mwanzo 5:17). Yaredi aliishi miaka 962 (Mwanzo 5:20). Enoki aliishi miaka 365 kabla Mungu kumchukua (Mwanzo 5:22-24). Lameki aliishi miaka 777 (Mwanzo 5:31). Mwanzo 9:29 imeandikwa kwamba Nuhu aliishi miaka 950.

Lakini mtu mkongwe zaidi katika Biblia, aliyeishi kuliko wengine wote ni mtu aitwaye Methusela, aliyeishi miaka 969 (Mwanzo 5:27). Huenda kulikuwa na mtu fulani kabla ya wakati wa gharika ambaye aliishi miaka mingi kuliko Methusela lakini Biblia haina habari za yeyote mwenye umri mkongwe zaidi. Ni machache sana yamesemwa kuhusu Methusela isipokuwa alikuwa babuye Nuhu. Kunazo maana mbili za jina lake Methusela: “Mtu wa mkuki” na “kifo chake kitaleta.” Kuna mapokeo mengine nje ya Biblia kwamba Enoki amabaye ni babake Methusela, alipewa ufunuo kutoka kwa Mungu kwamba gharika haingekuja hadi mwanawe afe. Ikiwa hilo ni kweli basi jina lake Methusela lingemaanisha “kifo chake kitaleta Gharika.”

Hesabu ya kibiblia inaunga mkono jambo hili kwa kuwa Methusela alifariki mwaka huo huo Gharika ilitokea. Methusela alimzaa Lameki alipokuwa na umri wa miaka 187 (Mwanzo 5:25). Lameki alimzaa Nuhu alipokuwa na umri wa miaka 182 (Mwanzo 5:28). Gharika ilitokea Nuhu alipokuwa na umri wa mika 600 (Mwanzo 7:6). 187 + 182 + 600 = 969, ambayo ndio umri wa Methusela alipokufa. Kwa hivyo huenda kukawa na hadithi ya kupendeza kuhusu Methusela, mtu wa umri mkongwe zaidi katika Biblia, na ni kwa nini aliishi miaka 969.

Kuna mambo machache sana tunayoweza kujua kwa uhakika kuhusu Methusela, mtu mkongwe zaidi katika Biblia. Aliishi miaka 969 na inaonekana alikufa mwaka huo huo Gharika ilipotokea. Alikuwa kitojo wa Adamu na babuye Nuhu. Yaonekana alikuwa mcha Mungu ambaye alibarikiwa na Mungu kwa kumpa maisha marefu.

[English]



[Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili]

Ni nani aliyekuwa mtu mkongwe zaidi katika Biblia?

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.