Nini maana na umuhimu wa kupaa kwa Yesu Kristo?

Swali Nini maana na umuhimu wa kupaa kwa Yesu Kristo? Jibu Baada ya Yesu kufufuka kutoka kwa wafu, “alijitokeza Mwenyewe” (Matendo 1: 3) kwa wanawake karibu na kaburi (Mathayo 28: 9-10), kwa wanafunzi Wake (Luka 24: 36-43), na wengine zaidi ya 500 (1 Wakorintho 15: 6). Katika siku zilizofuata kufufuliwa kwake, Yesu aliwafundisha wanafunzi wake…

Swali

Nini maana na umuhimu wa kupaa kwa Yesu Kristo?

Jibu

Baada ya Yesu kufufuka kutoka kwa wafu, “alijitokeza Mwenyewe” (Matendo 1: 3) kwa wanawake karibu na kaburi (Mathayo 28: 9-10), kwa wanafunzi Wake (Luka 24: 36-43), na wengine zaidi ya 500 (1 Wakorintho 15: 6). Katika siku zilizofuata kufufuliwa kwake, Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kuhusu ufalme wa Mungu (Matendo 1: 3).

Siku arobaini baada ya kufufuka, Yesu na wanafunzi wake walienda kwa Mlima wa Mizeituni, karibu na Yerusalemu. Hapo, Yesu aliahidi wafuasi wake kwamba hivi karibuni watapokea Roho Mtakatifu, na akawaagiza kubaki Yerusalemu hadi Roho atakapokuja. Kisha Yesu akawabariki, na alipokuwa akitoa baraka, akaanza kupaa mbinguni. Akaunti ya kupaa kwa Yesu inapatikana katika Luka 24: 50-51 na Matendo 1: 9-11.

Ni wazi kutoka kwa Maandiko kwamba kupaa kwa Yesu kulikuwa halisi, kurudi mbinguni kimwili. Aliinuka kutoka kwa aridhi polepole na kuonekana, alionekana na watazamaji wengi wenye nia. Vile wanafunzi walijikaza kushika mtazamo wa mwisho wa Yesu, wingu lilimficha kutoka kwa mtazamo wao, na malaika wawili walijitokeza na kuahidi kurudi kwa Kristo “jinsi iyo hiyo mlivyomwo akienda zake mbinguni” (Matendo 1:11).

Kupaa kwa Yesu Kristo ni wa maana kwa sababu kadhaa:

1) Ilionyesha mwisho wa huduma yake duniani. Mungu Baba alikuwa amemtuma Mwanawe duniani kwa upendo katika Bethlehemu, na sasa Mwana alikuwa anarejea kwa Baba. Kipindi chake cha upeo wa mwanadamu kilikuwa mwisho.

2) Ilionyesha ufanisi katika kazi Yake ya duniani. Yote aliyokuja kufanya, alikuwa amekamilisha.

3) Ilibainisha kurudi kwa utukufu wake wa mbinguni. Utukufu wa Yesu ulikuwa umefunikwa wakati wake duniani, isipokuwa kwa kifupi katika Mabadiliko (Mathayo 17: 1-9).

4) Ilionyesha kupandishwa kwake na Baba (Waefeso 1: 20-23). Yule ambaye Baba amependezwa sana naye (Mathayo 17: 5) alipokelewa juu kwa heshima na kupewa jina juu ya majina yote (Wafilipi 2: 9).

5) Ilimruhusu kutuandalia makao (Yohana 14: 2).

6) Ilionyesha mwanzo wa kazi yake mpya kama Kuhani Mkuu (Waebrania 4: 14-16) na Mpatanishi wa Agano Jipya (Waebrania 9:15).

7) Iliweka mpangilio wa kurudi kwake. Wakati Yesu atakapokuja kuanzisha Ufalme, atarudi jinsi alivyoenda, kihalisi, kimwili, na kwa kuonekana katika mawingu (Matendo 1:11; Danieli 7: 13-14; Mathayo 24:30; Ufunuo 1: 7).

Kwa sasa, Bwana Yesu yuko mbinguni. Maandiko mara nyingi humuonyesha kwenye mkono wa kulia wa Baba, nafasi ya heshima na mamlaka (Zaburi 110: 1, Waefeso 1:20; Waebrania 8: 1). Kristo ndiye Kichwa cha Kanisa (Wakolosai 1:18), mtoaji wa zawadi za kiroho (Waefeso 4: 7-8), na Mwenye anayejaza yote katika yote (Waefeso 4: 9-10). Kupaa kwa Kristo ilikuwa tukio ambalo lilibadilisha huduma ya Yesu duniani hadi huduma Yake ya mbinguni.

[English]



[Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili]

Nini maana na umuhimu wa kupaa kwa Yesu Kristo?

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.