Nitawezaje ili maombi yangu yajibiwe?

Swali Nitawezaje ili maombi yangu yajibiwe? Jibu Watu wengi wanaamini kwamba maombi yaliyojibiwa ni Mungu kukujibi ombi lo lote lilowekwa kwake. Kama ombi lo lote halikujibwa, inaeleweka kuwa ni maombi “yasiyo jibiwa.” Wakati mwingine Mungu jibu lake ni “la” au “ngoja.” Mungu anahidi pekee kuwa atatimiza majibu ya maombi yetu wakati tunauliza kulingana na mapenzi…

Swali

Nitawezaje ili maombi yangu yajibiwe?

Jibu

Watu wengi wanaamini kwamba maombi yaliyojibiwa ni Mungu kukujibi ombi lo lote lilowekwa kwake. Kama ombi lo lote halikujibwa, inaeleweka kuwa ni maombi “yasiyo jibiwa.” Wakati mwingine Mungu jibu lake ni “la” au “ngoja.” Mungu anahidi pekee kuwa atatimiza majibu ya maombi yetu wakati tunauliza kulingana na mapenzi yake. “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, yakuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwaba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba” (1 Yohana 5:14-15).

Inamaanisha nini kuomba kulingana na mapenzi ya mungu? Kuomba kulingana na mapenzi ya Mungu ni kuomba vitu ambavyo vinamheshimu na kumtukuza Mungu au kuomba chochote kile Bibilia inafunua kuwa ndio mapenzi ya Mungu. Kama tutaomba juu ya kitu fulani ambacho hakimweshimu Mungu ama chenye sio mapenzi ya Mungu katika maisha yetu, Mungu hatatupa chenye tunauliza. Tutawezaje kujua mapenzi ya Mungu? Mungu anahidi kutupa hekima wakati tunauliza. Yakobo 1:5 yasema, “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.” Mahali pazuri pa kuanzia ni 1 Wathesalonike 5:12-24, ambayo yaratibisha mambo mengi ambayo ni mapenzi ya Mungu kwetu. Tunavyo lielewa neno la Mungu zaidi, ndivyo tutakavyo jua chenye tutakavyo omba (Yohana 15:7). Tunavyo jua chenye tunaomba zaidi, ndivyo Mungu atakavyo kuwa na jibu la maombi kuwa “ndio.”

[English]



[Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili]

Nitawezaje ili maombi yangu yajibiwe?

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.