Upanga wa Roho ni nini?

Swali Upanga wa Roho ni nini? Jibu Maneno “upanga wa Roho” hupatikana mara moja tu katika Maandiko, katika Waefeso 6:17. Upanga ni sehemu ya silaha za kiroho Paulo anawaambia Waisraeli kuziweka ili kutuwezesha kupigana kwa ufanisi dhidi ya uovu (Waefeso 6:13). Upanga ni silaha yenye kukera na yenye kujitetea itumikayo kwa kujilinda kutoka kwenye madhara…

Swali

Upanga wa Roho ni nini?

Jibu

Maneno “upanga wa Roho” hupatikana mara moja tu katika Maandiko, katika Waefeso 6:17. Upanga ni sehemu ya silaha za kiroho Paulo anawaambia Waisraeli kuziweka ili kutuwezesha kupigana kwa ufanisi dhidi ya uovu (Waefeso 6:13).

Upanga ni silaha yenye kukera na yenye kujitetea itumikayo kwa kujilinda kutoka kwenye madhara au kushambulia adui na kumshinda. Ilikuwa ni lazima kwa mwanajeshi kupata mafunzo imara juu ya matumizi sahihi ya upanga wake ili kupata faida kubwa kutoka kwa hilo. Wanajeshi wote wa Kikristo wanahitaji mafunzo sawa imara ili kujua jinsi ya kushughulikia Upanga wa Roho, “ambalo ni neno la Mungu.” Kwa kuwa kila Mkristo ako katika vita vya kiroho dhidi ya nguvu za kishetani za ulimwengu huu, tunahitaji kujua jinsi gani ya kushughulikia Neno vizuri. Hapo basi itakuwa ni ulinzi wa ufanisi dhidi ya uovu na kosa la thamani ya “kubomoa ngome” za makosa na uongo (2 Wakorintho 10: 4-5).

Neno pia linaitwa upanga katika Waebrania 4:12. Hapa, Neno linaelezewa kama hai na tendaji na kali zaidi kuliko upanga wa kuwili. Upanga wa Kirumi kwa kawaida ulikuwa wa mara kuwili, na kuifanya vizuri zaidi kudunga na kukata njia zote mbili. Wazo la Maandiko kupenyeza inamaanisha kwamba Neno la Mungu linafikia “moyo,” katikati ya hatua, na inaweka wazi sababu na hisia za wale wanaoguswa nalo.

Madhumuni ya Upanga wa Roho-Biblia-ni kututia nguvu na kutuwezesha kukabiliana na maadui ya Shetani (Zaburi 119: 11, 119: 33-40; 119: 99-105). Roho Mtakatifu hutumia nguvu za Neno kuokoa nafsi na kuwapa nguvu za kiroho kuwa askari wakamilifu kwa Bwana. Bora tunayojua na kuelewa Neno la Mungu, ni muhimu zaidi kuwa tutafanya mapenzi ya Mungu na kwa ufanisi zaidi tutakuwa katika kusimama dhidi ya adui wa roho zetu.

[English]



[Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili]

Upanga wa Roho ni nini?

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.